Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kupeleka kombe lao Mlima Kilimanjaro

Yanga Kombe 2024 Gshs Yanga kupeleka kombe lao Mlima Kilimanjaro

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya tatu mfululizo, Klabu ya Yanga wamesema kuwa kesho wataanza safari ya kulipeleka kombe lao la ubingwa huo kwenye kilele mlima mrefu kuliko yote Barani Afrika, Mlima Kilimanjaro.

Hayo yamesemwa leo la Ofisa Habari wa Mabingwa hao wa muda wote (mara 30) wa Ligi Kuu ya Tanzania, Ally Kamwe baada ya kumalizika kwa ligi hiyo huku wakifanikiwa kumalizka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 80 na kupata tuzo ya mfungaji bora ambaye ni Aziz KI aliyefunga mabao matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.

“Kwanza kesho asubuhi na mapema tunakwenda kupeleka Kombe letu kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Wakati Ligi inataka kuanza kuna vitu vya hovyo sana vilipelekwa kwenye Mlima Kilimanjaro, sasa kesho tunakwenda kupeleka kitu cha maana kwenye Mlima Kilimanjaro.

“Yanga huwa hatusahau kama kuna kitu duniani kuna timu ina nongwa basi Yanga ni namba moja. Ukifanya jambo ujue hatusahau. Kesho Mwenyekiti wa wasemaji ninaanza safari ye kupeleka Kombe kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

“Kwa hiyo niwakaribishe mashabiki wa Yanga na wananchi wa mkoa Kilimanjaro, kesho saa 6 mchana ndege itakuwa imetua pale KIA, waje walipokee kombe lao, tunakwenda geti la Marangu, tunakwenda mpaka juu ya Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

“Tunataka tuwaoneshe dunia kwamba msimu ulipkuwa unataka kuanza ilikuwa kelele hizi, uchafu huu ukawekwa hapa na sisi Machampioni tumekuja kuweka mali yetu hapa,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live