Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuoga noti kufuzu Makundi CAF

Yangaa Hii Yanga kuoga noti kufuzu Makundi CAF

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga juzi ilikuwa uwanjani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo lakini vichwani kwao wanajua kwamba wamebakiza dakika 90 tu kuchukua mzigo wa Sh100 milioni kutoka kwa matajiri wao.

Iko hivi. Yanga ilipomalizana na Namungo tu akili zao haraka zimeanza kuwapigia hesabu wapinzani wao Al Merrikh ya Sudan katika mchezo utakaoamua nani anakwenda makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ndio iliyotanguliza mguu mmoja makundi baada ya ushindi mzuri wa mabao 2-0 ilioupata jijini Kigali, Rwanda ambako Wasudani ndiko walikochagua mechi zao za nyumbani zipigiwe huko.

Ushindi huo ni kama tayari mastaa wa Yanga wameshachukua nusu ya fedha, walizoahidiwa na matajiri wa klabu hiyo na kwamba wakiing’oa Merrikh watakabidhiwa fasta kiasi hicho cha Sh100 milioni.

Mbali na ahadi hiyo mastaa wa Yanga wanatambua kwamba bonasi hiyo itaongezeka zaidi katika mechi za hatua ya makundi ambapo kutakuwa na mgawanyo tofauti wa mechi za nyumbani na zile za ugenini watakazocheza.

Mmoja wa vigogo wa Yanga aliliambia Mwanaspoti kuwa, wameongeza dau kwenye hatua hiyo kwa lengo la kuhakikisha timu inafika mbali zaidi kwenye michuano hiyo ya CAF ambayo wana miaka 25 hawajawahi kutinga tena makundi tangu ilipofanya hiyo mwaka 1998 na kumaliza mkiani katika kundi walilopangwa.

Kigogo huyo (jina tunalo) alisema msimu uliopita wakati Yanga ikicheza Kombe la Shirikisho Afrika na kufika hadi fainali uongozi wa klabu hiyo ulifichua kwmaba kikosi chao kilitumia zaidi ya Sh1.5 bilioni kuwalipa bonasi pekee zilizochochea ushindi hadi ile ya mwisho ugenini dhidi ya USM Alger na kulikosa taji kwa faida ya bao la ugenini lililowabeba wenyeji baada ya matokeo ya mwisho kuwa sare ya 2-2.

Katika mechi ya kwanza nyumbani Yanga ilifungwa mabao 2-1 na kushinda ugenini 1-0 kwa bao la penalti la Djuma Shaban aliyepo Azam sasa akisubiri kutambulishwa dirisha dogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: