Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kumwaga zawadi mashabiki watakaopiga 'selfie' kwenye bango la 5G

Yanga Gj Yanga kumwaga zawadi mashabiki watakaopiga 'selfie' kwenye bango la 5G

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangaza kutoa zawadi ya jezi kwa mashabiki zake watakaopiga picha ya bango la 5G (kipigo cha Simba 1-5 Yanga) lililopo Barabara ya Ally Hassan Mwinyi na ku-post mtandaoni.

Huu ni mwendelezo wa Yanga kusherehekea ushindi wa bao 5-1 walizomkanda mtani wao kwenye mchezo wa Ligio Kuu ya NBC uliopigwa katika Dimba la Mkapa, Jumapili ya Novemba 5, 2023.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, Yanga wameandika; "Mwananchi kuwa wa kwanza kupiga picha kwenye bango la 5G Washindi wa kwanza 15 watajipatia uzi uliosainiwa na Wachezaji. Post picha yako sasa kisha tutag Instagram. Mnara unasoma barabara ya Ally Hassan Mwinyi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live