Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kumtangaza Okrah

Okrah Diarra Mn.jpeg Yanga kumtangaza Okrah

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga inatarajia kumtangaza mshambuliaji wa zamani wa Simba, Augustine Okrah ambaye ameonekana kufanya vizuri akiwa na klabu ya Bechem United ya Ghana.

Mshambuliaji huyo ambaye aliichezea Simba msimu wa 2022 na hakuweza kudumu nao, lakini alifunga bao mechi ya Kariakoo Derby kwenye Ligi Kuu Oktoba 23 mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1. 

Mwanaspoti imepata habari za uhakika tayari Okrah ametua nchini Tanzania, huku kikosi cha Yanga kikisafiri kesho hiyohiyo kwenda Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

"Yanga inamtangaza kesho (Desemba 29) baada ya kufika Zanzibar, Okrah baada ya kuondoka Simba na kurejea kwenye timu Bechem United ameonyesha kiwango cha juu," kilisema chanzo hicho

Amesema kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amepitisha jina la mchezaji huyo kwamba ataongeza nguvu kwenye kikosi chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live