Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kukipiga na Rivers bila Mashabiki

THE RETUNS YANGA Yanga SC

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Kihistoria klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) kuna kila dalili wakacheza mechi yao ya hatua ya awali ya Klabu bingwa katika Dimba la Mkapa bila ya kuhudhuriwa na Mashabiki.

Hatua hiyo inajiri baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kukataza mashabiki katika mechi zinazohusisha michuano yake.

Timu ambazo zina mechi mwezi huu ni Yanga ambao wanacheza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya River United ya Nigeria utakaochezwa kesho kutwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Biashara United na Azam FC ambao wanacheza Kombe la Shirikisho Afrika, ambao wanacheza leo.

Tayari klabu ya Azam FC kupitia msemaji wake Zakaria Thabit imeshakiri kupokea barua kutoka CAF inayowataka kucheza mechi hiyo bila kuruhusu mashabiki kuhudhuria viwanjani.

Akizungumza Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo amesema ni kweli Caf imezuia mashabiki viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona lakini TFF imeomba angalau waruhusiwe mashabiki kiasi lakini bado hawajajibiwa.

“Ni kweli Caf imezuia mashabiki viwanjani lakini TFF haijakaa kimya imeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) angalau mashabiki kiasi waruhusiwe lakini hadi sasa hatujajibiwa na endapo hatutajibiwa mechi zote zitachezwa bila mashabiki,” amesema Ndimbo.

Alisema mashabiki wasiwe na hofu kwani bado TFF inapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha wanapata kibali lakini ikishindikana basi maana hata mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Madagascar wa kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar waliomba lakini hawakuruhusiwa.

Kwa upande wa Yanga, msemaji wao Haji manara amesema mpaka sasa wameshaliandikia shirikisho la Mpira Afrika CAF barua tatu kupitia kwa TFF lakini hawajapewa majibu kama waruhusu mashabiki ama la.

Manara pia amesema kuhusiana na suala la Mashabiki watatoa tamko rasmi leo Ijumaa mchana baada ya swala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live