Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kukipiga na Cosmopolitan pale pale KMC Complex

Baleke Kiluvya Yanga kukipiga na Cosmopolitan pale pale KMC Complex

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuichapa Kiluvya Fc mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Manispaa ya Kinondoni jana, kesho Ijumaa Yanga itashuka tena katika uwanja huo kuikabili Cosmopolitan Fc inayoshiriki ligi ya Championship.

Muda wa mchezo huo ni saa 3 asubuhi kama ilivyokuwa mechi iliyopita dhidi ya Kiluvya Fc.

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amehitaji mechi hizo ili kuwapa 'game time' wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa.

Kwa sasa ni changamoto kwa Gamondi kukamilisha program za mazoezi ya kikosi chake kwa sababu anakosa nusu ya wachezaji wake ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa.

Kikosi cha Yanga kimesalia na takribani wachezaji 13 tu ambao wanaongezewa nguvu na wachezaji kutoka timu ya vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live