Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kukaa meza moja na Fei Toto

Feisal Salum Fei Toto Malengo Yanga kukaa meza moja na Fei Toto

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema kuwa watahakikisha hakuna mchezaji mzuri ataondoka katika Klabu hiyo yenye makazi yake Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Hersi amesema kuwa wanaendelea na michakato kuwaongezea mikataba wachezaji ambao mikataba yao imebakiza muda mfupi.

Akizungumza kuhusu suala ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’, Injinia Hersi amesema kiungo huyo fundi ataendelea kuitumikia Yanga kwa kuwa bado ana mkataba wa muda mrefu.

Amesema kama uongozi jukumu lao la kwanza ni kuhakikisha wachezaji wao wazuri hawaondoki.

Ameongeza kuwa uongozi utakaa nae chini kuboresha mkataba wake ili aendelea kuitumikia klabu hiyo.

“Nataka niwahakikishie. Hakuna mchezaji mzuri ambaye ataondoka katika klabu ya Yanga, tufute hiyo kwenye akili zetu”

“Feisal ataendelea kusalia Yanga na tutakaa nae kwa ajili ya kuboresha na kuongeza mkataba wake sio msimu huu ila 2024 baada ya mkataba wake kumalizika”

“Feisal ni mchezaji muhimu kwetu, hakuna uwezekano wa yeye kuondoka. Hilo hatutakubali. Hatusemi hivyo kwa sababu tunataka kutumia nguvu ili abaki, ni kwa sababu tunayo NEGOTIATION POWER.

“Amefanya vizuri akiwa na sisi na sisi lazima tumpe thamani anayostahili”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live