Yanga inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Augsburg ya Ujerumani itakayochezwa Afrika Kusini keshokutwa Jumamosi.
“Yanga tarehe 20 (mwezi huu) anakwenda kucheza na Augsburg ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki, Augsburg ambayo baada ya maandalizi hayo atakwenda kucheza na Bayern Munich, Yanga atarudi kushughulikia watu kwenye Ligi ya Mabingwa.” Ofisa Habari Yanga SC, Ally Kamwe.
Mchezo huo ambao mashabiki wengi wa soka wanasubiri kuwaona mastaa Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Clatous Chama wakicheza pamoja kwa mara ya kwanza.
Chama ametua Yanga dirisha hili kuongeza nguvu kwa mabingwa hao watetezi ambao wanajipanga upya kwa msimu wa 2024/2025.