Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuivaa Biashara United

Yanbiashara Pic Data Yanga kuivaa Biashara United

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIKOSI cha Yanga kinaendelea na mazoezi katika kambi yao iliyopo Kigamboni kwenye viwanja vya Avic.

Yanga wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ambao utachezwa Aprili 11, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema awali walikuwa wacheze mechi ya kombe la (Azam Sport Federations Cup), dhidi ya Tanzania Prison Aprili 4, katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

Alisema ratiba ilikuwa inaonyesha wanatakiwa kucheza mechi ya ASFC, dhidi ya Prison lakini imeahilishwa kutokana na maombelezo ya msiba wa Kitaifa yatamalizika Aprili 7.

"Siku hiyo Aprili 7, ambayo maombelezo yanamalizika tulitakiwa kucheza mechi ya ligi na KMC ambayo kwa hali ya kawaida haitaweza kuchezwa nayo itasogezwa mbele kama ilivyokuwa ile ya ASFC," alisema Saleh.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz