Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuimaliza mechi kwa Mkapa Dar es Salaam

MSEMAJI MANARA Msemaji wa Yanga, Haji Manara

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Septemba 12, siku ya Jumapili Klabu ya Yanga itashuka dimbani Uwanja wa Mkapa kutafuta ushindi katika mchezo wa hatua ya awali ya Klabu bingwa Afrika dhidi ya Rivers United kutoka kule nchini Nigeria.

Tayari Yanga kwa mujibu wao wamekwishafanya maandalizi yote ya msingi ndani na nje ya uwanja.

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kushiriki hatua hizi za awali za ligi ya Mabingwa Afrika na kwa kulitambvua hilo safari hii wamekuja na mpango mkakati wa kuhakikisha wanamaliza shughuli mapema ili angalau wanapokwenda ugenini wasiwe na kazi kubwa.

Akizungumzia mipango hiyo Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema, mpango wao ni kushinda goli nyingi ili watakapokwenda ugenini basi iwe kazi rahisi kwao.

"Lengo letu ni kutumia vyema uwanja wa nyumbani ili tushinde angalau goli nne, tuwe na mtaji mkubwa linapokuja suala la kwenda ugenini basi kila kitu kisiwe kigumu kwetu"

"Tuko vizuri, amini tuko vizuri ndani na nje ya uwanja, kimwili na kiakili na matayarisho yote yapo tayari ni suala la kusubiri siku tu" amesema Manara

Yanga imekumbana na changamoto ya kuzuiliwa wachezaji wake watatu wa kimataifa beki Shaban Djuma, Khalid Aucho na Kiungo Fiston Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live