Yanga inapiga hesabu nzito za kufunga usajili na mshambuliaji ambaye ndiye mtu muhimu anayehitajika na kocha wao Miguel Gamondi.
Yanga inaendelea na msako wa mshambuliaji gani wamchukue ndani ya siku chache zilizosalia kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Dirisha dogo la usajili linafungwa Januari 15 ambapo kila timu inahaha kukamilisha maeneo hayo muhimu ya ufungaji kulingana na mapungufu waliyonayo.
Rais wa Yanga injinia Hersi Said amekaririwa akithibitisha kwamba kikosi chao kitafunga usajili kwa kumuingiza mtu mmoja ingawa hakutaka kutaja nafasi Mwanaspoti linafahamu anayekuja ni mshambuliaji.
"Usajili bado na tutamleta mchezaji mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa, amesema Hersi wakati akihojiwa na vyombo vya habari baada ya hafla ya Harambee ya timu za Taifa wiki hii.
Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu za Afrika kwasasa yupo nchini Ivory Coast ambako amekwenda kuhudhuria mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).