Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kufunga usajili na chuma hiki leo

Mamadou Doumbia Mamadou Doumbia

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa leo majira ya saa 5:59 usiku. Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limesistiza hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya dirisha kufungwa.

Vilabu vimetakuwa kukamilisha usajili pamoja na 'Uhamisho' wa Kimataifa kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi.

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili, kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Kennedy Musonda. Hata hivyo bado kuna utambulisho wa mchezaji mmoja unasubiriwa.

Kulingana na Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe ambaye alibainisha kuwa watafunga dirisha dogo la usajili kwa kutambulisha wachezaji wawili wa Kimataifa, ambao ni Mshambuliaji (Musonda) na mlinzi wa kati.

Tetesi zinaeleza kuwa Yanga imelamilisha usahili wa mlinzi wa kati Mamadou Doumbia kutoka Mali katika klabu aliyowahi kuitumikia mlinda lango namba moja wa Yanga, Djigui Diarra.

Pengine kabla ya dirisha kufungwa saa 5:59 usiku, beki huyo anaweza kutambulishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live