Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kufikisha 5G tisa leo dhidi ya Geita?

Yanga Tano Pacome Maxi 191929 Yanga kufikisha 5G tisa leo dhidi ya Geita?

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kugawa dozi kwa vijana wa Mbogo Maji Ihefu FC kwa goli 5-0, Wananchi Yanga SC wanashuka dimbani leo kuwakabili wachimba dhahabu Geita Gold FC kusaka ushindi wa 5G ya tisa kwa msimu huu, mechi itakayochezwa pale Azam Complex Chamazi majira ya Saa 2:15 Usiku.

Ushindi au sare katika Mchezo wa leo utaifanya Yanga SC kufikisha mechi 15 mfululizo bila kupoteza ambapo katika michezo 14 iliyopita imeshinda mechi 13 na kutoa sare 1.

Geita Gold FC ambayo imekuwa haifanyi vizuri katika mechi 14 zilizopita katika ligi kuu, imeshinda michezo minne, imetoka sare nne na kupoteza mechi sita ikishika nafasi ya 13 ikiwa na alama 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live