Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya tatu mfululizo, Klabu ya Yanga wamesema kuwa watafanya parade ya kiatu cha ufungaji bora baada ya mchezaji wao, Aziz Ki kutwaa tuzo hiyo kwa kufikisha mabao 21 mbele ye fei Toto mwenye mabao 19.
Hayo yamesemwa leo la Ofisa Habari wa Mabingwa hao wa muda wote (mara 30) wa Ligi Kuu ya Tanzania, Ally Kamwe baada ya kumalizika kwa ligi hiyo huku wakifanikiwa kumalizka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 80 na kupata tuzo ya mfungaji bora ambaye ni Aziz KI aliyefunga mabao matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.
“Tulikuja kufuata kiatu chetu hapa leo, tunakwenda kuandaa parade la kiatu cha ufungaji bora. Si mnasema Yanga tunapenda sifa? Sisi ni Mamlaka ya Sifa Duniani, tunaenda kuandaa parade ya kiatu. Tutawasiliana na TFF kujua wataandaa wapi tuzo kama ni Zanzibar au dar es Salaam wajue Wananchi tutatoka na Parade letu hapo mpaka Jangwani.
“Mwaka huu kama walidhani shughuli zimeisha ndiyo kwanza zimeanza, kuna parade ya kiatu imeanza. Leo Yanga imetoa mfungaji bora na kufikisha mabao 108 kwenye mashindano yote na bado mchezo mmoja.
“Leo nimefurahi kwanza Aziz amekuwa top-scorer tena kwa gepu kubwa, tumepata MVP na Aziz Ki anachukua tena tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei, jumla ni tuzo nne za mwezi anachukua kwa mwaka mzima,” amesema Kamwe.