Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuchomoa straika Saudi Arabia

Glody Kilangalanga Glody Kilangalanga

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga imefanya jaribio zito la kumchukua mshambuliaji mmoja Mkongomani ikiendelea na msako wa kutafuta mashine ya mabao katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili Tanzania Bara

Mabosi wa timu hiyo wametua kwa straika wa timu ya Bisha FC ya Saudi Arabia, Glody Kilangalanga ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu huu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo ambaye wanaamini atawafaa.

Straika huyo mwenye nguvu ya miguu na kujua kufunga, bado ana mkataba na timu hiyo ambayo alitua akitokea CS Chebba ya Tunisia, ambapo Yanga inataka kufanya biashara moja kati ya mbili ama kuuziwa au kupewa kwa mkopo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wanaamini kwamba Kilangalanga hajaanza kutumika kwa kasi ndani ya timu hiyo nafasi ambayo Yanga inataka kuitumia baada ya kuonekana kukwama kuwanasa washambuliaji iliowataka.

Awali, Yanga ilikuwa inawawinda Sankara Karamoko ambaye klabu ya Asec Mimosas imeweka ngumu kumuachia baada ya kuanza kuibuka viashiria vya dili nyingi za nje ya Ivory Coast.

Mbali na Sankara, pia Yanga ilikuwa imefikia patamu kumpata mshambuliaji Ranga Chivaviro wa Kaizer Chiefs, lakini kocha wa muda wa timu hiyo, Cavin Johnson akaweka ngumu kutoa baraka za straika huyo kuondoka.

Jaribio lingine la Yanga lilikuwa kwa Saimon Msuva ambaye amedengua kuwapa jibu la uhakika mabosi wa timu hiyo, huku mshambuliaji huyo akiamiani kuwa bado anaweza kupata dili zuri nje ya nchi baada ya Fainali za Mataifa Afrika (Afcon 2023) kumalizika.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi anadaiwa kubakiza kupokea watu wawili kwenye kikosi wakiwa ni mshambuliaji wa kati na winga wa kulia ambayo ndio mahitaji yake kwa sasa.

Tayari Yanga imemsajili Shekhan Ibrahim Khamis kutoka JKU na Augustine Okra aliyekuwa Benchem FC ya Ghana.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: