Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kucheza Mbele ya Mashabiki 30,000 wa Al Ahly

Pacome Yanga Al Ahly.jpeg Yanga kucheza Mbele ya Mashabiki 30,000 wa Al Ahly

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyanzo vya habari Misri, vimefichua Al Ahly imeruhusiwa kuingiza mashabiki 30,000 kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Cairo, Misri.

Al Ahly itaikaribisha Yanga kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi zikiwa kundi D, baada ya mchezo wa kwanza timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi, utapigwa Ijumaa ijayo kuanzia saa 1:00 usiku na miamba hiyo inasaka kumaliza nafasi ya kwanza ambayo Al Ahly ndiyo inashikilia kwa sasa ikiwa na pointi tisa huku Yanga ikiwa ya pili na pointi nane, Wanajangwani wanasaka ushindi kwenye mechi hiyo ili kumaliza kinara kwenye kundi hilo.

Vyanzo vilifichua kuwa African Giants wamepata kibali kutoka kwa mamlaka ya usalama kuruhusu mashabiki 30,000 kuhudhuria mechi hiyo ambayo inazikutanisha timu zote zikiwa zimeshafuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Al Ahly ilitinga robo fainali baada ya kuifunga Medeama bao 1-0 huku Yanga ikifanya hivyo kwa kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 katika mechi za raundi ya tano.

Al Ahly wenyewe wanahitaji hata sare katika mechi hiyo ili kujikita kileleni mwa Kundi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: