Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuanzia ugenini Makundi Ligi ya Mabingwa

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga kuanzia ugenini Makundi Ligi ya Mabingwa

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lunyasi eeeh, mnaanzia nyumbani kisha mtamalizia nyumbani. Hamna ratiba nzuri kama hii kwenye mashjndano ya Kimataifa.

Imarisheni kiungo pale wapinzani wanawin sana second balls sasa hii kwenye makundi mkiendelea kuruhusu itakuwa ngumu kutoboa.

Vinginevyo hamna kundi gumu, hao watatu wote mlishakutana nao, mkawafunga wakawafunga, so njia za kupita mnazijua na uzoefu mnao. Jambo kubwa ninalolisubiria kwenu ni kumuuliza swali yule Jwaneng Galaxy na akose majibu.

Wananchi eeeh. Mnaanzia ugenini na kumalizia ugenini. Siku za hivi karibuni mmekuwa mwiba ugenini hivyo ratiba bila shaka haiwatishi.

Mna hesabu kubwa sana lakini hakikisheni mnachukua tisa kutoka kwa Medeama na Belouizdad. Mtazipata vipi nyie wenyewe mnajua cha kufanya maana sio watoto tena.

Ila jitahidini kuimarisha ile safu yenu ya ushambuliaji, sio kila mechi mtakuwa mnapata nafasi nyingi, kwenye makundi zipo nyakati chache mtapata nafasi kiduchu na mtalazimika kuzitumia hizo hizo.

Halafu kwa namna yoyote msiruhusu hatima yenu isubiri mechi ya mwisho. Malizeni shughuli mapema na mechi dhidi ya Al Ahly iwe angalau ya kuamua mshindi wa kundi.

Sawa inawezekana wamepungua ubora ila wakubwa zaidi yenu wale na huwa hawakawii kutibua mambo.

Mtazamo wangu wa jumla, kundi la kifo ni lile C lenye timu za Esperance, Petro Luanda, Al Hilal na Etoile du Sahel. Maisha ya kambale hapo kila mtu ana ndevu.

Halafu linafuatia kundi A la Mamelodi, Pyramids, TP Mazembe na Nouadhibou na likitoka hilo linakuja kundi la Yanga na kisha kundi la Simba.

Tarehe zilizothibitishwa za mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa:

Siku ya kwanza ya mechi: Novemba 24 na 25, 2023

Siku ya pili ya mechi: Desemba 1, 2, 2023

Siku ya tatu ya mechi: Desemba 8, 9. 2023

Siku ya mechi ya nne: Desemba 19, 2023

Siku ya mechi ya tano: Februari 23, 24, 2024

Siku ya mechi ya sita: Machi 1, 2, 2024.

Kwa makundi waliyopangwa Yanga na Simba unawapa asilimia nagapi ya Kufuzu? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: