Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuanza kambi rasmi ya 'pre-season' Julai 8, Avic Town

Yanga WA0042 Yanga kuanza kambi rasmi ya 'pre-season' Julai 8, Avic Town

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangaza kuwa Jumatatu ya Julai 8, mwaka huu, wachezaji wa timu hiyo wanatarajia kuanza kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema siku hiyo wachezaji wote wakiwemo wapya na wale wa zamani watatakiwa kufika Avic Town kwa ajili ya kukutana.

Baada ya hapo, benchi la ufundi la Young Africans SC chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, litaanza mikakati ya kuiandaa timu.

"Young Africans SC tumekuwa na malengo makubwa zaidi msimu ujao ambayo ni kutetea mataji yetu mawili ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Federation tuliyobeba 2023-2024, pia kurudisha taji letu la Ngao ya Jamii.

"Mbali na hayo, pia tunahitaji kufika mbali zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita kuishia robo fainali," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live