Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kimyakimya yashusha vifaa vipya

Yanga Tf Yanga kimyakimya yashusha vifaa vipya

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa wamekuja kivingine katika aina yao ya usajili ambao wameanza kuufanya kimyakimya huku ikiwa imemalizana na baadhi ya nyota wapya huku ikiwaboreshea mikataba wachezaji swao wa zamani.

Yanga ilianza kwa kumsajili winga wa TP Mazembe, Phillipe Kinzumbi ambaye anayetajwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kimyakimya.

Timu hiyo, haikuishia hapo haraka wakafanya maboresho ya mikataba ya nyota wake muhimu wanaotarajiwa kuimaliza mapema mwishoni mwa msimu huu.

Baadhi ya nyota hao ni Dickosn Job na Khalid Aucho ambao wote mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku wakiendelea kuiboresha kwa wengine.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa kabla ya Ligi Kuu Bara kumalizika usajili wao wao utakuwa umekamilika kwa asilimia mia moja kuelekea msimu ujao.

Bosi huyo alisema kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi tayari ametimiziwa mahitaji ya wachezaji ambao amewahitaji kwa ajili ya kuwasajili kimyakimya kati ya hao yupo beki wa kulia Datius Peter anayeichezea Kagera Sugar ambaye anasifika kwa kupiga krosi ‘kumwaga maji’.

Aliongeza kuwa pia wapo wachezaji wengine wa kigeni wanaocheza Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika majina yao ni siri, kwani hivi sasa wapo katika taratibu za mwisho za kuipata saini zao.

“Yanga wamekuja kivingine katika aina yao ya usajili, kwani kwa asilimia mia moja wamekamilisha usajili wa wachezaji wao wapya waliokuwepo katika mipango ya kocha Nabi.

“Uzuri kwamba Nabi mwenyewe amehusika katika usajili huo baada ya kutoa mapendekezo ya wachezaji anaowahitaji, ambao tayari wamesajiliwa kimyakimya kwa hofu ya kuingia katika ushindani wa kugombea mchezaji.

“Hivyo kabla ya ligi kumalizika ninaamini usajili kwa ajili ya msimu ujao utakuwa umekamilika kwa asilimia mia moja, baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa ni Kinzumbi na Datius ambao usajili wao umekamilika kimyakimya na wapo wengine wanakuja wa kigeni,” alisema Bosi huyo.

Akizungumzia usajili hiovi karibuni, Rais wa timu hiyo, Injnia Hersi alisema kuwa: “Tumepanga kukifanyia maboresho makubwa kikosi chetu kwa gharama yoyote.

“Tutahakikisha kila mchezaji atakayependekezwa na kocha kwa ajili ya kusajiliwa, basi ni lazima tufanikishe usajili wake,” alisema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: