Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kazi kazi Nigeria

Yanga WA0056 Yanga kazi kazi Nigeria

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya kwanza ya ufundi katika Jimbo la Uyo, ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United.

Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF siku ya Jumapili majira ya saa 8:00 kwa saa za hapa Nigeria.

Wananchi ambao wamekita kambi yao kwenye hoteli ya Sheraton, wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa Akwa, mazoezi yalioshuhudia na Rais wa Yanga Eng Hersi Said na Makamu wake, Arafat Haji.

Mazoezi hayo yaliodumu kwa saa 1:30 yalilenga kujenga utimamu wa wachezaji lakini muda mwingi kocha mkuu Nasredinne Nabi alijikita kwenye kutoa maelekezo ya mbinu juu ya jinsi ya kuwakabili Rivers United.

Viongozi wengine wa Yanga walioshuhudia mazoezi hayo ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Alex Ngai na Munir Said.

Kabla ya kuanza mazoezi kwa siku ya leo, Rais wa Yanga Hersi Sais alianza kwa kuwakumbusha wachezaji umuhimu wa mchezo wa Jumapili na ni nini mashabiki wanakitarajia kutoka kwao.

“Mashabiki wana imani kubwa sana na nyie, tumepoteza Derby lakini wamekuwa sambamba na nyie kwa sababu wanaamini mnakwenda kuwapa rekodi ya kucheza Nusu Fainali ya Afrika,” alisema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: