Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kama jeshini, Nabi akaza uzi

Khali Aucho Kh Yanga kama jeshini, Nabi akaza uzi

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amebadili programu yote ya mazoezi ya timu hiyo kuanzia asubuhi ya leo.

Tofauti na awali ambako mastaa wa timu hiyo walikuwa wakipiga matizi mara moja tu kwa siku sasa wametangaziwa utaratibu mpya ambapo watalazimika kupasha mara mbili kwa siku. Asubuhi wataamkia kwenye mazoezi ya gym kwenye viwanja ghali vya Gymkhana na jioni watakiwasha Avic Town Kigamboni.

Nabi anasema kwamba lengo la mazoezi hayo ni kurudisha utimamu wa miili ya wachezaji hao kuendana na mechi inayofuata ambayo ni dhidi ya Biashara kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) wiki ijayo.

Kocha huyo aliyeanza kuzungumza maneno kadhaa ya Kiswahili, amesisitiza kwamba anataka wachezaji wake wakirejea uwanjani wawe na kiwango kikubwa na wasiache pointi hata moja.

Alisema kwamba watasimama mazoezi hayo ya nguvu siku chache kabla ya mechi hiyo ili wachezaji wakae sawa tayari kukiwasha kwenye mechi hizo ngumu za kimkakati ambazo hawapaswi kupoteza hata moja kwani wanataka kurejesha hadhi ya Yanga kwa kukusanya makombe mengi msimu huu.

Nabi ameliambia Mwanaspoti kwamba anataka ushindani katika kikosi chake lakini kuhusu winga wake mpya Denis Nkane ambaye hajaonekana muda mrefu ni kwamba ana maumivu lakini mbali na kuwa majeruhi kuna shida ameigundua.

Alisema bado hajaridhishwa na mwanzo wa Nkane ndani ya kikosi chake na amekutana naye na kumwambia ana deni kubwa ndani ya jezi za klabu hiyo.

Kocha huyo alisema Nkane bado ni kijana mdogo na kwamba kama atajiona ni staa mkubwa ni rahisi kupotea ndani ya kikosi hicho.

“Napenda kufanya kazi na vijana, unajua vijana wana nguvu, najua ana maumivu lakini bado sijaridhika na mwanzo wake katika timu nafikiri sasa atakuwa amenielewa.

“Alianza vizuri lakini baada ya kufunga kule Zanzibar kuna aina ya maisha ya kuridhika yamemuingia akilini, hii sio nzuri kwake nimemwambia yeye (Nkane) bado ni mchezaji mchanga asidhani ni staa mkubwa.

“Yanga imemuamini kuja hapa, anachotakiwa ni kutihibitisha kwamba sisi makocha hatukukosea kumleta hapa, anatakiwa kupigania namba kwa nguvu na sio kuwa wa kawaida tena.

“Nimemwambia wakati huu ana maumivu ajiandae kiakili ili akirudi tu awe Nkane tofauti anayekuja kupigania nafasi na sio kuridhika kuwaona wenzake wakicheza,” alisema Nabi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz