Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga itamkanda Al Ahly - Shabiki Simba

Yanga Janja Janja.jpeg Yanga itamkanda Al Ahly - Shabiki Simba

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa kutokana na ubora wa kikosi cha timu Yanga, anaamini watamfunga mpinzani wao Al Ahly kwenye mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchome amesema hayo baada ya kuona uwezo wa Yanga tangu msimu ulivyoanza wakiifunga Simba bao 5-1 licha ya kufungwa na CR Belouizdad ya Algeria katika mchezo wa kwanza ya hatua ya makundi ya CAFCL.

"Kocha Benchikha ana profile nzuri sana na mara nyingi Simba kinachotugharimu ni profile. Yani namba za watu huwa zinatudanganya sana kwenye suala la usajili. Tumemsajili Onana, alikuwa MVP huko alikotoka, tumemsajili Che Malone alikuwa MVP kule alikotoka lakini wako wapi? Wanapoteana.

"Matokeo ya Yanga hayajafichwa na matokeo mabaya ya Simba. Kabla Simba hajacheza, Wananchi walikuwa na furaha kwa sababau timu yao imefungwa lakini imonyesha mpira mzuri. Shida ya Simba sio kutoa sare ni kutoonyesha mpira mzuri.

"Yanga wamefungwa lakini ball posession iliongoza, mashuti wanaongoza, kona inaongoza hadi faulo inaongoza, backline imefanya kazi yake vizuri mno, wameongoza kila idara.

"Timu kama hiyo ikifungwa unawalaumu vipi? Yanga wana haki ya kujisifia na matumaini kwamba mechi ijayo wanakwenda kushinda kutokana na kile walichoonesha.

"Ninaamini Yanga atamfunga Al Ahly, kama Simba ilivyo mbovu lakini imetoka nae sare kwa Mkapa na kule kwao, Yanga ametufunga sisi bao tano, anashindwaje kumfunga Ahly? Anamkanda kabisa, na mimi nitakuwepo kushangilia mabao ya Pacome, Maxi," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: