Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga itakuwa klabu ya kwanza kuleta Kombe la CAFCL nchini - Shabiki Simba

Yanga Shamra Yanga itakuwa klabu ya kwanza kuleta Kombe la CAFCL nchini - Shabiki Simba

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa Klabu ya Yanga ndiyo itakuwa ya kwanza kuleta Kombe la Mabingwa Afrika hapa nchini kutokana na uwezo wao wanaouonesha hivi sasa.

Mchome amesema kuwa, Yanga wanatekeleza malengo yao kwa vitendo kuanzia viongozi, watendaji wao, wachezaji na hata mashabiki tofauti na watani zao Simba ambao amedai kuwa wamekuwa wakicheza mpira 'mdomoni' badala ya uwanjani.

Kauli hiyo ya Mchome inakuja baada ya Yanga kuonesha kiwango bora kwenye mechi za kimataifa na kufanikiwa kumfunga CR Belouizdad kwa bao 4-0 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Kinachowapa mafanikio Yanga ni kuwa na wafanyakazi wenye mapenzi na timu yao, ni kuwa na wafanyakazi mashabiki wa timu yao, sio wafanyakazi wanaoshabikia mifuko yao na familia yao, wale ni timu kwanza, mafanikio yao binafsi ni baadaye.

“Yanga itakiwa klabu ya kwanza kuleta kombe la mabingwa Afrika hapa nchini na si klabu nyingine yoyote. Kamwe alipata presha maana ilikuwa si kawaida kumfunga CR Belouizdad, ni furaha kubwa sana,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live