Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga itacheza nusu fainali ya CAFCL kabla ya Simba - Oruma

Yanga Musonda010 Yanga itacheza nusu fainali ya CAFCL kabla ya Simba - Oruma

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, kupitia EFM, Wilson Oruma maarufu kama Mzee wa Jambia amesema kuwa, Klabu ya Yanga ndiyo itakuwa timu ya kwanza nchini kucheza hatua nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya wapinzania wao Simba SC.

Oruma amesema hayo mara baada ya Yanga wakiwa ugenini kushinda mchezo wao wa CAFCL dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan kwa bao 2-0 huku Simba wakitoa sare dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia.

“Amini nakwambia, Young Africans wanaweza wakacheza Nusu Fainali ya CAF Champions league mapema zaidi kuliko Simba Sc. Ndani ya misimu mitanop Simba amecheza nusu fainali mara nne (tatu CAFCL na moja CAFCC), akaweka standard kwamba ndiyo timu ambayo imefanikiwa zaidi hapa nchini kwenye michuano ya Kimataifa.

“Lakini Yanga wamekuja msimu uliopita, lengo lao ikawa kufika hatua ya Makundi, lakini wakaenda mpaka fainali. Kitu pekee kilichowanyima Yanga kuwa mabingwa wa CAFCC ni kanuni,” amesema Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live