Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga inayokuja usipime

Yangasc 290568475 412384414154538 563027722022495542 N Kikosi cha Young Africans msimu wa 2021/2022

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mgombea makamu wa Rais katika klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema endapo akifanikiwa kushinda nafasi hiyo atafanya makubwa ya kwa kushitikiana na wenzake.

Amesema kama wajumbe watamchagua anataka kulifanya soka liwe la kisasa kwa kuanza kushindana kimataifa kwa mafanikio makubwa.

"Tutatengeneza timu imara iliyojaa wachezaji wenye viwango vya juu, benchi imara lenye wataalamu katika sekta mbalimbali kama watu wa kufanya data za wachezaji". amesema na ameongeza;

"Tutaandaa mikakati ya timu za vijana wenye vipaji vikubwa na kuweka mikakati ya namna ya kuwapandisha timu ya wakubwa, hilo litatokana na uchumi imara". amesema,

"Tutatafuta wadhamini wa timu hizo ambao hawatakuwa wanaingiliana na wa timu kubwa, hilo litafanya tuwe na timu za vijana imara na zenye malengo makubwa".

Mbali na hilo, amesema wataboresha timu  ya wanawake kwa kuwa na kikosi cha U-17, ili kukuza vipaji vitakavyoleta tija kwenye timu za taifa.

Related Uchaguzi Yanga wapamba moto Suma ajivunia kipigo Simba"Tumepata chachu ya kuwekeza nguvu kwenye timu za wanawake baada ya kuona timu ya taifa ya U-17 kufuzu kucheza Kombe la Dunia, hivyo Yanga tunahitaji kikosi chetu kiwe na wachezaji mahili wa kulitumikia taifa lao,"amesema.

Ukiachana na hilo, amesema wataifanya Yanga iwe na nguvu kimataifa kuhakikisha wanapocheza michuano ya CAF wanachukua taji.

"Yote hayo yatatokana na kusajili wachezaji na kuwa na benchi imara kama nilivyosema awali naamini yote hayo yatawezekana kama tutapata nafasi ya kupitishwa na wajumbe kwa kura nyingi"amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz