Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Oscar Oscar amesema kuwa ubora wa kikosi cha Yanga SC ni ule ule kama msimu uliopita, hivyo Kocha Gamondi amepata bahati ya kuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri kikosini hapo.
Oscar amesema hayo kufuatia matokeo chanya ambayo Yanga imekuwa ikiyapata kwenye michezo yake tangu msimu huu umeanza licha ya kiondokewa na baadhi ya nyota wake pamoja na aliyekuwa kocha wao Mkuu, Nasreddine Nabi.
"Umeitazama vizuri Manchester City ya Pep Guardiola katika Ligi Kuu ya pale England namna ambavyo imekuwa katika ubora wake ule ule huu unaenda msimu wa tatu sasa.
"Sasa ule ubora wa Manchester City ndio huu ubora ambao Yanga wako nao katika Ligi Kuu ya NBC huu ukiwa unaenda msimu wa tatu. Azam FC na Simba ambao ndio washindani wakubwa wa Yanga ila wamekuwa na vipindi vya mpito.
"Kuna nyakati Simba wanakuwa bora katika mechi tano ama sita alafu wanapoteana kama ambavyo Azam fc walivyo.
"Mabingwa wa nchi Yanga wanaendelea kulitawala soka letu katika Ligi Kuu kwa sababu ubora wao haupungui,katika mechi 10 wanaweza wakafanya vibaya mechi moja ndiyo maana unawaona wameweza kushinda mataji manne katika hii misimu miwili," amesema Oscar.