Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ina majibu alipo Mukoko

IMG 20210222 181915 Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Baada ya kuzagaa taarifa za kiungo mkabaji wa Yanga, Mkongomani, Mukoko Tonombe hayupo na kikosi hicho kambini nchini Morocco, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela, ameibuka na kutaja alipo kiungo huyo.

Yanga ikiwa kambini nchini Morocco, watu wamekuwa wakihoji alipo Mukoko kutokana na kushindwa kuonekana kwenye picha za mazoezi ambazo mastaa wote wameonekana kasoro yeye.

Hofu kwa Wanayanga juu ya kiungo huyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa dili la kusajiliwa na RS Berkane ya Morocco ambayo hivi karibuni imewasajili Tuisila Kisinda na Clatous Chama.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwakalebela alisema, Tonombe hakuonekani katika picha za pamoja za mazoezi yaliyofanyika juzi kutokana na kuuguza majeraha.

Mwakalebela amesema kuwa, kiungo huyo ana program maalum akiifanya na beki wa kati wa timu hiyo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

“Wanayanga waondoe hofu juu ya mchezaji wao Tonombe, wafahamu kuwa bado ni mchezaji wetu na msimu ujao atakuwa sehemu ya wachezaji wa Yanga.“

Tonombe kambini anaendelea na mazoezi kama kawaida, lakini yeye na mwenzake Ninja wana program maalum za mazoezi ya binafsi.

“Hiyo ndiyo sababu ya wao kutoonekana katika picha za pamoja na wachezaji wenzao wakiendelea na mazoezini".

Chanzo: globalpublishers.co.tz