Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imeweka rekodi nyingine kwa Simba baada ya miaka 8

Aziz Ki Simba Yanga Yanga imeweka rekodi nyingine kwa Simba baada ya miaka 8

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Simba kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya watani zao wa jadi Yanga mabao yaliyofungwa na Aziz Ki pamoja na Joseph Guede huku bao la Simba likifungwa na Freddy Michael, ushindi huo Yanga unawafanya kuirudia rekodi yao walioiweka msimu wa mwaka 2015/16 kwa kuwafunga Simba nyumbani na ugenini katika ligi kuu.

Kwenye msimu huo Septemba 20 mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga wakiwa nyumbani waliifunga Simba mabao mawili yaliyofungwa na Amiss Tambwe dakika ya 44 kabla ya Malimi Busungu kufunga dakika ya 79.

Mchezo wa pili Yanga wakiwa ugenini Februari 20 2016 waliifunga tena Simba mabao mawili ya Donald Ngoma dakika 39 kabla ya Amiss Tambwe kufunga dakika ya 72.

Msimu huu wa 2023/24 yamejirudia tena baada ya Novemba 5, 2023 Simba wakiwa nyumbani walikula chuma tano kwa moja kabla ya kufungwa tena mabao mawili kwa moja kwenye mchezo wa marejeano ambao Yanga walikuwa nyumbani uliopigwa April 20 2024 kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live