Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imetumia milioni 200 kuwafuata Mamelodi

Yanga 1170x650.jpeg Kikosi cha Yanga

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga Engineer Hersi Said ameeleza gharama ya safari ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwenye mechi klabu bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakayochezwa leo Ijumaa.

Hersi akiongea na chama cha waandishi habari wa Afrika Kusini (SAFJA) amesema safari yao inagharimu Dola za Kimarekani 80,000 (Tsh Milioni 206)

“Ni gharama sana kuendesha klabu ya mpira wa miguu. Ninaweza kukuambia safari yetu kuja Afrika Kusini kucheza na Mamelodi inagharimu USD 80,000” — Amesema Hersi

“Tiketi ya kwenda na kurudi (kwa mtu mmoja) ni USD 600. Na nimekuja na watu 50. Hiyo ni USD 30,000. Watu 50 mara USD 150 kwa siku, zidisha kwa siku nne. Hiyo ni USD 30,000 nyingine.

“Hapo hujanunua kitu chochote na gharama za hoteli. Unatakiwa kuzunguka hapa na pale. Baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupewa posho wanaposafiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live