Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imetoka mbali nyie!

Gnamien Gislain Yikpe.jpeg Yanga imetoka mbali aisee

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 2020 Yanga SC wakiwa wanajitafuta walibahatika kupata striker jitu mwitu msitu kutoka Ivory coast, Yikpe Gislain ambaye alifunga mabao mawili tu akiwa Yanga na kukosa nafasi kama 50 hivi.

Nakumbuka alisajiliwa kutoka Gor-Mahia ambapo aliondoka kwa sababu ya kutolipwa mshahara, alipotua Yanga SC viongozi walimtaka afanye majaribio, akakataa, akasajiliwa bila trials.

Kilichofuata the rest is history.

19-21 Yanga ilikuwa na washambuliaji hawa na ilitegemea kufanya vizuri kimataifa

◉ Yikpe Ganamien Gislain.

◉ Ditram Nchimbi.

◉ Juma Balinya.

◉ Michael Sarpong.

◉ David Molinga Ndama.

◉ Sadney Khoitege.. nk

Hapo nyuma 2017-21 Yanga SC wali struggle sana kupata wachezaji bora sio kwa sababu hawakuwa na scouting nzuri, hapana.

Hawakuwa na pesa;

Nakumbuka walishakubaliana kuwasajili wachezaji hawa lakini mwishoni wakaenda Simba SC kwa sababu walikuwa hawana pesa ya kushindana na Mo Dewji ambaye aliingia Simba SC 2018 mwaka ambao Yusuph Manji (RIP) aliondoka Yanga SC na kuwaacha Yanga wakiwa yatima.

◉ Meddie Kagere.

◉ Luis Miquisson.

◉ Clatous Chama.

◉ Raly Bwalya.

Tofauti na sasa, pesa ipo (GSM) na mtu mwenye maono yupo (Hersi Said ) ndio maana wanapata Wachezaji bora kutoka kwenye vilabu vikubwa Afrika tofauti na zamani wachezaji waliwatoa EAC.

Kwa sasa East Africa nzima wachezaji wa Yanga ndio wanauliziwa zaidi sokoni na vilabu vikubwa Afrika. Hali hiyo haijaja kwa bahati mbaya ni kwa sababu walisajili Wachezaji bora ambao wanafanya vizuri.

Hujiulizi kwa nini vilabu vingine Tanzania Wachezaji wao hawagombaniwi sokoni !?

Hapo nyuma Yanga walisajili wachezaji wengi wenye profile ya chini kutoka vilabu vidogo kwa sababu ya ukata | Bakuli.

◉ Juma Balinya - Police FC - Uganda

◉ Yikpe Gislain - Gor-mahia - Kenya

◉ Michael Sarpong - Rayon sports - Rwanda

◉ Patrick Sibomana - APR - Rwanda

◉ Farouk Shikalo

◉ Sadney Urikhob - Without club.

Wachezaji wa sasa wa Yanga walipotoka:

◉ Djigui Diarra - Stade Malien - Mali

◉ Yao Kouassi - ASEC Mimosas - Ivory Coast

◉ Pacome Zouzoua - ASEC Mimosas - Ivory Coast

◉ Aziz Ki - ASEC Mimosas - Ivory Coast

◉ Khalid Aucho - Masr El Makasa

◉ Max Nzengeli - Union Maniema - Congo DR

◉ Jean Baleke - TP Mazembe - Congo DR.

◉ Clatous Chama - Simba

◉ Chadrack Boka

◉ Prince Dube

◉ Duke Abuya

◉ Kennedy Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live