Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imeshusha watano, kaeni tayari kuanzia leo

CD445CF7 28DD 485D 9347 147C16CA2E09.jpeg Viongozi wa Young Africans

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema Yanga imesajili nyota watano wa kigeni ambao wataanza kuwatambulisha leo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili wakitokea Arusha walikocheza mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam na kutwaa taji kwa kumfunga Coastal Union kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1 baada ya sare ya mabao 3-3.

Manara anasema wamesajili wachezaji watani tu wa kimataifa na wanaanza kumtambulisha mmoja lsaa 6 usiku.

“Ni wachezaji watano tu wa kigeni hatujasajili mchezaji yeyote mzawa na usiku wa kuamkia Jumatatu tuna mtangaza mmoja, kuamkia Jumanne, Jumatano mmoja hadi wanatimia watano,” anasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live