Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imenifundisha kuwa-bingwa - Mshery

Mshery 682 Yanga imenifundisha kuwa-bingwa - Mshery

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba mbili wa kikosi cha Yanga, Aboutwalib Mshery, amesema alichojifunza ndani ya Young Africans ni kuwa bingwa na kuendelea kupambania ndoto.

Kauli ya Mshery imekuja ikiwa hii ni mara yake ya tatu mfululizo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC tangu alipoanza kuvaa jezi ya Young Africans Desemba 2021.

“Msimu huu ulikuwa mzuri sana, tumepambana kutoka mwanzo mpaka hapa leo tumechukua ubingwa kwa sababu mwisho wa msimu unatakiwa kuwa na kitu na kitu chenyewe ndio hiki kwa hiyo ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu.

“Ndani ya Yanga nilichojifunza ni kuwa bingwa, nashukuru sana kwa hilo,” alisema Mshery.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: