Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imefyeka kichaka cha Simba

Simba Yanga WA0007 Yanga imefyeka kichaka cha Simba

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binafsi sikuona ulazima wa Klabu ya Simba SC kuizungumzia Yanga SC mbele ya wanahabari na kupost kwenye kurasa zao rasmi.

Badala yake wangezungumzia mambo yanayohusu Simba SC pekee kuelekea mechi muhimu ya kufuzu robo fainali dhidi ya Jwaneng kwa sababu kauli hizi zinawatoa mashabiki wa Simba, wanahabari na wadau katika lengo mama la mkutano huo na kuanza kujadili Yanga SC.

Agenda ya mkutano ilikuwa Jwaneng, mashabiki kujitokeze lakini kwa sasa katika platform zote inazungumzwa Yanga SC. Wamewapa Yanga Airtime ya bure bila kulipia.

Nukuu ya Meneja wa Habari Simba SC, Ahmed Ally;

“Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Mo Dewji na wa pili ni Simba SC. Wakati Mo Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua.

"Baada ya miaka 5 ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza ya Yanga wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi,” amesema Ahmed Ally

Kauli hizi zinatoa tafsiri nyingi, hii ni miongoni mwa hizo nyingi;

Wivu na maumivu; Kitendo cha Yanga SC kuingia robo fainali CAF-CL tukio hilo limefyeka kichaka kilichotumika kujifichia kwamba "Yanga hawajawahi kuingia robo fainali".

Kichaka hicho kilitumika kwa miaka mingi kudharau mafanikio makubwa ya Yanga SC hata walipofika fainali CAF-CC, kuwa na makombe mengi ya ligi kuu (29) nk... kinapofyekwa kichaka ulichozoea kujifichia kama 'defensive mechanism' lazima uumie (maumivu) na uone wivu (wivu).

Klabu ya kwanza Tanzania kucheza group stage CAF-CL & CC ni Yanga SC. Haya waliyafanya kipindi Mo Dewji akiwa hafikiriwi kama atakuja kuwekeza Simba SC. Mo Dewji ashukuriwe pia?!

Mo Dewji alikuja Simba kipindi ambacho Yusuph Manji anaondoka Yanga (2018) baada ya kutawala soka la Tanzania akiwa kwenye mchakato wa kufanya Mabadiliko kutoka kuwa Yanga asili kuwa kampuni ili klabu iifanye vizuri kimataifa that's why Yanga aliingia group stage CAF-CC mara 2 katika misimu (3). Sababu ya kuondoka inafahamika.

Kuondoka kwa Manji ilikuwa ni fursa kwa Mo Dewji kutawala soka la Tanzania na kujikita kwenye lengo alilolihubiri Manji (Kufanya vizuri kimataifa) akafanikiwa huku wenzao Yanga wakirudi nyuma (Bakuli).

Ujio wa (GSM) ulikuja kuendeleza ndoto ya Yusuph Manji na Yanga SC Kufanya vizuri kimataifa na kwa 70% wanaelekea kufanikiwa.

Kusema Yanga SC wameingia robo fainali wakushukuriwa ni Mo Dewji na Simba ni kauli iliyojaa wivu, maumivu na dharau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live