Timu bora imeshinda mechi, simple like that hata hizo goli tatu walizofunga APR kwa Yanga ni basi tu hawakuwa na matumizi mazuri ya nafasi walikuwa wanaweza kupata zaidi ya haya mgaoli.
Kuanzia dakika ya 10 ulikuwa mchezo wa kupishana sana na Yanga waliweza kuutawala mchezo hadi kupata matokeo ya kuongoza ila APR waliendelea kusukuma mashambulizi na walifanikiwa kupata goli la kusawazisha.
Walichofanya APR baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili walifanya kitu ambacho timu nyingi hufanya ili kupata matokeo mazuri zaidi mbele ya Yanga ni kuendelea kusukuma mashambulizi bila kukata tamaa.
1: APR pale kati waliwaweka Christian, Fils na Ruboneka ili kufanya pressing dhidi ya Mauya, Chigombo na Farid ambapo walifanikiwa mno hasa kipindi cha pili.
2: Yanga walizidiwa mno pale katika ambapo Mauya, Chigombo na Farid walikuwa wanaacha space kubwa ya kushambuliwa.
3: Gilbert, Ruboneka na Fils wanufaika na eneo la kati la Yanga kuacha space kubwa pale wanapoporwa mpira walikuwa hawarudi kutrack back mapema.
Yanga kwenye eneo la Midfield walikatika mno na kushindwa kutrack back kwa kuwasaidia walinzi nyuma ambao walikuwa wanakutana na 3v2 hadi 3v1.
APR walipiga pasi okay tu na kufanya runs za hatari mno kwenye mpira na kuzitumia nafasi walizotengeneza kutokana na runs zao dhidi ya Yanga.
NOTE
1: Yule golikipa wa APR ambae ni Pavelh anajua mno kunusa hatari, kulinda lango na ni mtulivu mno.
2: Gift Fred alifanya kazi kubwa mno pale nyuma.
3: Chigombo, Nanguka na Tamila hawa kweli wanaweza kuhimili 90 kwenye mechi kubwa?
4: Ruboneka amewapika mno viungo wa Yanga.
5: Yule beki wa kulia wa APR ambae ni Solomon alikuwa na game nzuri mno pia utulivu wake kichwa.
FT: Yanga 1-3 APR.