Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ikitimiza Miaka 87 leo, Mafanikio na Umri vinawiana?

Yanga Miaka 87 Kikosi cha Yanga cha msimu wa 2021-2022

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga iliyopo chini ya Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla na timu yake leo Februari 11 imefikisha miaka 87 tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 1935, huku ikiwa na mafanikio kedekede ya kujivunia na kukumbukwa.

Mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu ya Bara ikiwa imebeba taji la ligi hiyo, hilo mara 27 huku wapinzani wao Simba ikibeba mara 22.

Yanga msimu huu ni kama imezaliwa upya kutokana na usajili walioufanya baada ya kukosa ubingwa kwa misimu minne mfululizo, ikipewa nguvu kubwa na GSM, Sportpesa, Taifa Gas, na wadhamini wa Ligi NBC na Azam Media.

Timu hiyo imetoa wachezaji wenye majina makubwa na mafanikio kama Boniface Mkwasa, Sunday Manara ambaye ndio alikuwa mchezaji wa kwanza Tanzania kucheza soka kulipwa nje mwaka 1978 kwenye ligi ya Uholanzi.

Wananchi ndio timu ya kwanza Tanzania kushiriki michuano ya kimataifa ya CAF, ikicheza Klabu BIngwa Afrika mwaka 1969 na kufika robo fainali ikitolewa na Asante Kotoko ya Ghana na kurudia tena 1970.

Pia ndio klabu ya kwanza nchini kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 baada ya kubadilishwa mfumo 1997 na Kombe la Shirikisho Afrika 2016 na 2018 baada ya kumaliza nafasi za mwisho katika makundi na kuondolewa kwenye mashindano hayo.

Kundi A ambalo lilikuwa na timu za Yanga, TP Mazembe, Mo Bejaia na Madeama SC mnamo mwaka 2016 ambapo Yanga ilifanikiwa kushinda mchezo mmoja, sare 1 na vipigo mara 4.

Lakini haikuishia hapo Yanga ndio timu inayoongoza kuliwakilisha taifa la Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ikiwa ni Klabu bingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika na kombe la Kagame.

Ikumbukwe Yanga ndio timu pekee nchini imefanikiwa kutwaa mataji ya Kombe la Kagame nje ya ardhi ya Tanzania ikifanya hivyo, 1993 na 1999 nchini Uganda huku ikitwaa kombe hilo mara 5.

Mafanikio ya Yanga toka imeanzishwa

Kombe la Ligi Kuu Bara-27 Kombe la FA-5 Kombe la Kagame-5 Kufika robo fainali klabu bingwa Afrika-1969 na 1970 Kufuzu hatua ya Makundi kombe la Shirikisho Afrika-2016 na 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live