Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika watafanya kweli kama ilivyokuwa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Imemaliza mwendo hatua ya makundi ikiongoza kundi D na kibindoni ina pointi 13 mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya TP Mazembe iliposhinda kwa bao 0-1 ikiwa ugenini.
Meneja wa Yanga, Walter Harrison ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Dhamira yetu ilikuwa ni kushinda na kukamilisha hesabu tukiwa tunaongoza kundi, kwa hatua ambayo tumefikia sio mbaya tunahitaji kuwa na mwendelezo mzuri kwenye hatua ya robo fainali.
“Mipango ipo vizuri na tunaamini tutaendelea kufanya vizuri kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani tunaamini mambo mazuri yanakuja.”
Yanga imepangwa kukutana na Rivers United ya Nigeria katika hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.