Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga huenda wasianzie 'Preliminary' Ligi ya Mabingwa msimu ujao

Yanga Out CAF Yanga huenda wasianzie 'Preliminary' Ligi ya Mabingwa msimu ujao

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao 2024|2205, Klabu ya Yanga inaweza isianzie hatua ya awali (Preliminary round).

Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) timu (10) za juu kwenye viwango vya ubora (CAF) hazianzii preliminary round kwenye Ligi ya Mabingwa.

Currently club Ranking:

01. Al-Ahly Cairo - Misri (82)

02. Esperance de Tunis - Tunisia (61)

03. Wydad Casablanca (60) - Morocco (hatashiriki)

04. Mamelodi Sundowns (54) - Afrika Kusini

05. Zamalek - Misri (43) - (hatashiriki)

06. RS Berkane (42) - Morocco (hatashiriki)

07. Simba SC (39) - Tanzania (hamna uhakika)

08. Petro Atletico - Angola (39)

09. TP Mazembe - Congo DR (38)

10. CR Belouizdad - Algeria (37)

11. USM Alger (36) - Algeria (hatashiriki)

12. Raja Casablanca - Morocco (35)

13. Young Africans SC - Tanzania (31)

14. ASEC Mimosas - Ivory Coast (30)

Kwa nini wasianzie Preliminary Stage?

Klabu (4) zenye (X) zilizo juu ya Yanga SC kwenye viwango vya (CAF) hapo kwenye list hazitashiriki ligi ya Mabingwa Afrika 24|25, wanaenda Shirikisho (CAF).

Maana yake ukizitoa timu hizo Yanga anaingia kwenye top (10) ya timu bora ambazo zina qualify kutoanzia hatua ya awali Preliminary round CAF champions league msimu ujao 2024|2025.

Yaani:

01 ◉ Al-Ahly Cairo - Misri

02 ◉ Esperance de Tunis - Tunisia

03 ◉ Mamelodi Sundowns - Afrika Kusini

04 ◉ Simba SC (Hakuna uhakika) - Tanzania

05 ◉ Petro Atletico - Angola

06 ◉ TP Mazembe - Congo DR

07 ◉ CR Belouizdad (Algeria)

08 ◉ Raja Casablanca (Morocco)

09 ◉ Young Africans (Tanzania)

10 ◉ ASEC Mimosas (Ivory Coast)

Iwapo Simba asipofuzu kushiriki ligi ya Mabingwa Afrika timu nyingine iliyo nyuma ya ASEC Mimosas itaingia top (10) na kupata sifa ya kutoanzia preliminary round.

Pia Young Afticans SC wakiingia group stage watawekwa kwenye POT (B) tofauti na POT (C) walipokuwa last season.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live