Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hofu tupu kuivaa Tanzania Prisons

Yanga Picha Kikosi cha Yanga, chakumbwa na majeruhi

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania maarufu kama ASFC baina ya Yanga na Ihefu, klabu hiyo imetoa taarifa kuwa itakosa huduma ya wachezaji wanne kuelekea mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Ihefu ASFC, inategemea kucheza na Prisons Jumapili ikiwa bado ni kinara wa Ligi hiyo.

Wachezaji ambao wamekuwa na shida tofauti tofauti katika klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na majeruhi ni Fiston Mayele, Kibwana Shomari, Yacouba Sogne na Yusuf Athumani.

Kwenye mchezo huo, Yanga mabao yake yalifungwa na Heritier Makambo akiingia kambani mara tatu na Khalid Aucho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live