Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hizi sasa ni sifa

Yanga Bingwa Sisri Yanga hizi sasa ni sifa

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amesema Bodi ya Ligi na wadhamini wa ligi hiyo NBC wamewaandalia sherehe kubwa za ubingwa zitakazofanyika Mei 25 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kamwe amesema tukio hilo litakuwa la kihistoria kwenye soka la Tanzania.

“NBC benki bora Tanzania kwa kushirikiana na bodi ya ligi wametuandalia sherehe ya ubingwa. Kama inakuuma na wewe kapambane nawe uwe bingwa kwama unahisi ni rahisi. Tunasherehe kubwa haijawahi kutokea party kubwa ya ubingwa barani Afrika,” amenukuliwa Kamwe.

Siku chache zilizopita Yanga walitangazwa mabingwa wa ligi kwa mara ya tatu mfululizo na huo unakuwa ni ubingwa wa 30 wa Ligi Kuu katika historia yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live