Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hii unapigwa kwa namna nyingi

Mudathir Yahaya Abbas Yes Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahaya

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa namna Yanga ilivyo na kikosi kipana na kumiliki mastaa wanaoweza kuhudumu zaidi ya nafasi moja, kinapunguza presha ya benchi la ufundi kufanya kazi yao chini ya Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedrick Kaze.

Mwanaspoti limebaini ndani ya kikosi cha Yanga wapo mastaa wanaoweza wakafanya majukumu nje ya namba zao halisi na wakatekeleza kile wanachoagizwa na makocha wao.

Mfano mzuri ni kile alichokifanya staa wao mpya, Mudathir Yahya kucheza namba 10 kwenye mechi dhidi ya TP Mazembe, Yanga ikishinda mabao 3-1, kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

Imezoeleka kumuona Mudathir akicheza namba 6, 7, 8, tofauti na na siku hiyo akicheza kwa mara ya kwanza namba 10, ambayo akikosekana mtu kama Aziz Ki anaweza akaziba pengo.

Mastaa wengine wa kikosi hicho ambao wana uwezo wa kuziba mapengo ya wenzao ni Stephen Aziz Ki licha ya kucheza namba 10 pia anaimudu 11, pia anaweza kucheza namba 8, anayocheza Dickson Ambundo anayemudu kucheza nafasi zote za winga, Bernard Morrison 10, 11, Farid Mussa ana uwezo wa kucheza beki wa kushoto, winga na kiungo mshambuliaji, Jesus Moloko anaweza kucheza 7,11, Yanick Bangala 5,6 na beki wa pembeni, Shomari Kibwana 2,3 na Kennedy Musonda amekuwa akicheza 7,9 ambayo akikosekana Fiston Mayele timu inakuwa na uhakika wa kufunga.

Mchezaji mwingine wa Yanga anayemudu kucheza nafasi nyingi tofauti kwa ufasaha ni Dickson Job ambaye anaweza kucheza nafasi ya beki wa kati lakini pia beki wa kulia na kiungo namba sita.

Ukiachana na Yanga ambayo ina mastaa wengine kwenye kikosi cha kwanza wanaocheza nafasi nyingi, Simba haijawa nyuma katika hilo ingawa wengi wao hawaanzi na wengine wamekosa namba kabisa, kuna wanaocheza nafasi zaidi ya moja.

Kwa upande wa Simba kuna kiraka Erasto Nyoni anaweza kucheza beki na kiungo, Kibu Denis kuna wakati anapangwa kushambulia kuanzia pembeni na kati 10, 11, Nassoro Kapama 5,6 mwenye nafasi finyu kwenye kikosi hicho.

Wengine ni Habib Kyombo anayemiliki mabao mawili anacheza 9,11, Ousmane Sakho 7,10 na Said Ntibazonkiza 'Saido' ambaye ana mabao 10 lakini pia Clatous Chama ambaye amekuwa akicheza namba 10 na wakati mwingine anaweza kucheza winga wa pembeni.

Kwa namna mastaa hao wanavyoweza kunyumbulika kocha wa timu ya vijana wa Simba, Mussa Hassan Mgosi alisema soka la kisasa linahitaji mchezaji anayejiongeza kama kucheza zaidi ya nafasi moja.

"Soka ni biashara kubwa duniani, mchezaji akicheza zaidi ya nafasi moja akawa kwenye kiwango cha juu ni rahisi kuwania na kila timu inayohitaji kufanya vizuri na thamani yake ikawa kubwa," alisema.

Kwa upande wa kocha Nabi, alisema anawajenga wachezaji wake kucheza zaidi ya nafasi moja na wengi wao wanatimiza majukumu kama inavyotakiwa, akitolea mfano wa alichokifanya Mudathir dhidi ya TP Mazembe.

"Mchezaji anatengenezwa, naamini akiwa tayari anaweza akacheza kwenye nafasi nyingi na kwa kiwango kizuri,"alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live