Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hii, kumbe bado haijakamilika

Nabi Pic Data Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi akitoa maelekezo kwa wachezaji

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbona kama wamepania. Ndio kauli unayoweza kusema baada ya Kocha mkuu wa Kikosi cha Yanga, Nasreddine Nabi kudai kuwa anafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakamilisha kile alichokiomba kwa uongozi wa Yanga apewe siku 90 atengeneze timu.

Yanga haikuwa na maandalizi mazuri kuelekea kuanza kwa msimu huu jambo ambalo lilionekana kuwaathiri kwa kiasi kikubwa wakati wa mechi zao kwani waliahirisha kambi yao ya maandalizi kule nchini Morocco, baada ya wachezaji wao kukumbwa na janga la Corona.

Wachezaji wao wengine hasa wa kigeni walichelewa kujiunga na timu na hivyo wakakosa kufanya maandalizi yanayoeleweka.

Kwa sababu hizo walijikuta wanapoteza mechi dhidi ya Rivers United nyumbani na ugenini na kutolewa katika hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa siku chache tangu Yanga wawe pamoja kama kikosi chini ya Nabi tayari wameshacheza mechi 6 za kimashindano ndani ya nchi, na zote wameibuka na ushindi na sio tu ushindi bali wametandaza soka la kitabuni, soka safi.

Walianza kwa kumchapa mtani wake wa Jadi, Simba SC, katika pambano la ngao ya Jamii Septemba 25, ambapo walishinda bao 1-0, goli la Straika mpya kunako kikosi hicho Fiston Mayele.

ukija kwenye Ligi Kuu wanongoza msimamo wakiwa kileleni na alama zao 15 baada ya kucheza michezo mitano na kuibuka na ushindi katika michezo yote hiyo.

wameshinda dhidi ya Kagera sugar ugenini, Geita Gold nyumbani, KMC ugenini, Azam nyumbani kisha wakamaliza na Ruvu Shooting nyumbani.

Kwa aina ya mpira wanaocheza Yanga kila mtu anatamani kuiona ikicheza, wanacheza soka la burudani.

Sasa Kocha wa Yanga, Nabi anasema hicho kinachooneshwa na Yanga hivi sasa ni kipindi cha mpito kuelekea aina ya soka ambalo anahitaji kikosi chake kicheze.

Nabi amesema anajaribu kutoa maelekezo ya msingi ili kila kitu kikae kama anavyohitaji ndani ya wiki chache zijazo.

Nabi bado hajakaa akatulia kwa kua anaona namna ambavyo anataka Yanga icheze bado hajaridhika nayo japo amekiri anaona mabadiliko makubwa ndani ya kikosi.

Tusubiri kuona ni aina gani ya soka ambalo watacheza baada ya mwalimu kuridhika kwa kile anachowapa wachezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live