Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hawapoi, wajichimbia kuisoma Singida Big Stars

Yanga Shirikisho Yanga hawapoi, wajichimbia kuisoma Singida Big Stars

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze leo Novemba 15, amesema pamoja na uchovu waliokuwa nao wachezaji wao na ratiba kuwabana lakini wamejipanga kuhakikisha keshokutwa Alhamisi wachukua pointi tatu dhidi ya Singida Big Stars.

Akizungumza, kocha huyo amesema kikosi chao kimeingia kambini leo asubuhi Avic Town Kigamboni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wanajua utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wao lakini lengo lao ni kuzibakisha Jangwani pointi zote tatu.

“Nimchezo mgumu sababu ratiba imekuwa ngumu kwetu tumekuwa tukicheza mechi kila baada ya siku mbili lakini haina namna lazima tucheze na lazima tushinde kwanza tunataka pointi tatu lakini jambo la pili ni kuhakikisha tunailinda rekodi yetu ya kutopoteza mchezo kwenye ligi,” amesema Kaze.

Kocha huyo amesema leo asubuhi wamefanya mazoezi ya Gym na jioni watafanya mazoezi ya uwanjani na kesho watafanya mazoezi kwa awamu moja pekee ya asubuhi kwa ajili ya kuuandaa mwili kabla ya mchezo huo siku ya Alhamisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live