Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali amesema kuwa Klabu ya Yanga haina uwezo wa kumlipa kiungo mshambuliaji wa Taifa Stars, Simona Msuva kwani mshahara wake ni mkubwa kuliko uwezo wa klabu hiyo.
Kauli hiyo ya Boiboi imekuja mara baada ya Msuva ambaye aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa kisha kutimkia uarabuni ambapo juzi alidai kuwa amemaliza mkataba na timu yake ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia hivyoa anapokea ofa za ndani na nje ya nchi.
"Simon Msuva alikuwa ankusanya Mshahara wa kiasi cha Dola 12000 kwa wiki ambazo ni sawa na kiasi cha Tsh milioni 28 za Kitanzania, Kwa ujumla kwa mwezi akusanya Dola 50,000 ambazo ni sawa na kiasi cha shillingi Milioni 117 za Kitanzania.
"klabu ya Yanga imekuwa ikihusishwa na kumsajili Simoni Msuva kutokana na Mchezaji huyo kumaliza kwa Mkataba wake na klabu yake ya Al Qadasiah ya nchini ya Saud Arabia," amesema Boiboi Mkali.