Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hawajapiga tizi tangu washinde

Majukumu Yanga Yanga hawajapiga tizi tangu washinde

Sat, 20 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Yanga jana alfajiri kiliwasili katika uwanja wa Julius Nyerere Terminal 3 kikitokea nchini Afrika Kusini ilipokwenda kushinda mchezo wa pili wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Marumo Gallants.

Imefuzu fainali ya Kombe hilo baada ya kuifunga Marumo jumla ya mabao 4-1 ikiwa mchezo wa kwanza hapa Tanzania kushinda 2-0 kisha kwenye marudiano huko Afrika Kusini kushinda 2-1.

Baada ya kuwasili kikosi hicho kila mchezaji alipewa mapumziko madogo ya kwenda kuiona familia yake kisha kurejea kambini kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam dhidi ya Singida Big Stars.

Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze akizungumzia ratiba alisema tangu wamecheza mechi yao na Marumo siku ya Jumatano, hawajawa na mazoezi ya kutosha kutokana na namna ambavyo Safari yao ilivyokuwa.

“Wachezaji waliocheza kwa dakika 90 kwenye mechi yetu hawajapata muda mzuri wa kupumzika, nazani inawezekana kukawa na mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza; “Tutaondoka hapa na ndege hadi Dodoma kisha tutakuwa na mwendo wa gari takribani masaa matano unaona kabisa Safari itakavyokuwa.”

“Hii ndio maana ya kuwa na kikosi cha pili chenye nguvu kwani hata anapokosekana fulani basi mwingine yupo.”

ALITAKA KOMBE CAF

Kaze alisema baada ya kutinga fainali ni wazi kabisa anajua mchezo utakuwa mgumu lakini wanajiamini.

Kaze alisema anajua watacheza na USM Alger fainali ya Shirikisho na imani yake watapambana kuhakikisha wanataka na ubingwa.

“Ukifika hatua hii hakuna mechi rahisi lakini uzuri kuna nyumbani na ugenini, kikubwa ni kujiamini na hilo linatufanya tutachukua huu ubingwa.”

Chanzo: Mwanaspoti