Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hatua moja mbele kufanikisha usajili wa Staa wa Asec Mimosas

IMG 4442 Zoungrana.jpeg Mohammed Zoungrana

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zanadai Timu ya Yanga wapo katika hatua nzuri kukamilisha dili la usajili wa mchezaji Mohammed Zoungrana raia wa Ivory Coast ambaye anacheza klabu ya Asec mimosas ya nchini Ivory coast.

Tayari mazungumzo baina ya Yanga na Asec mimosas yameshafanyika juu ya makubalino ya ada ya usajili Asec mimosas wamekubali kuwaruhusu Yanga kufanya/Kuanza mazungumzo na menejimenti ya mchezaji Mohammed Zoungrana, bado ana mkataba na klabu yake mwaka mmoja hadi June 30,2024

Uongozi wa Yanga kuanzia wiki ijayo rasmi wataanza mazungumzo na menejimenti ya mchezaji Mohammed Zoungrana "Nass Footbal Management" kufanikisha dili hilo.

Mchezaji Stephanie Aziz KI amehusika sehemu kubwa sana ya dili hilo, Mohammed Zoungrana na Stephanie Aziz KI wote walicheza pamoja Asec mimosas msimu wa mwaka 2021-2022 kwa mafanikio makubwa.

Je Yanga watafanikisha dili hili? Unauzungumziaje usajili huo? Tuachie maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: