Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hasira zote kwa Azam FC "Tukutane Zenji Mei 2"

Yangas Aziz Kiii Yanga hasira zote kwa Azam FC "Tutaondoka Alhamisi"

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya tatu mfululizo, Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa Kikosi cha timu hiyo kitaondoka Alhamisi kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB utakaopigwa Jumapili, Juni 2, katika Dimba la Amaan dhidi ya Azam FC.

Kamwe amesema hayo baada ya kumalizika kwa ligi hiyo huku wakifanikiwa kumalizka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 80 na kupata tuzo ya mfungaji bora ambaye ni Aziz KI aliyefunga mabao matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.

“Tunaondoka hapa Alhamisi (Mei 30, 2024) kwenda Zanzibar kwa ajili ye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC. Na uzuri wachezaji wetu wanajua umhimu wa hii mechi, juzi nilimsikia kapteni wetu Dickson Job akisema kwamba wanafahamu wameacha deni kubwa kwa mashabiki.

“Tunakwenda tukijua tunacheza na Champions League mwenzetu, ni fainali ya hadhi sio confederation Cup, nii ni fainali ya hadhi ya CAF Champions League,” amesema Kamwe.

Itakumbukwa msimu, msimu huu Yanga wamekutana na Azam mara tatu ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa nusu fainali ya Ngao ya Jamii ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, mechi ya pili ilikuwa ya duru la kwanza la Ligi Kuu, yanga ilishinda kwa mabao 3-2, mabao yote ya yanga yakifungwa na Aziz Ki.

Mchezo wa tatu uliopigwa Machi 17, 2024 ambao ulikuwa wa duru la pili la Ligi Kuu, Azam iliibuka ushindi wa mabao 2-1, hivyo Wananchi wana hasira ya kulipa kisasi kwa wauza ukwaju hao wa Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live