Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hakuna kulala,Gamondi awapa mastaa programu maalumu

Miguel Gamondi Programme Yanga hakuna kulala,Gamondi awapa mastaa programu maalumu

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, hana mchezo mchezo, kila mchezaji atakaporejea kutoka mapumziko atalazimika awe katika ufiti unaotakiwa, kutokana na programu alizowapa.

Gamondi amegawa programu, kulingana na kile walichokifanya wachezaji msimu ulioisha, wapo ambao watachukua muda mrefu katika mapumziko na wale ambao watatakiwa wafanye kazi ya ziada kujiweka fiti, ili msimu mpya utakapoanza wawe na uwiano wa kuonyesha kiwango bora.

Katika mazungumzo yake na Mwanaspoti, alitolea mfano wa Attoula Yao jinsi ambavyo alitumika sana msimu ulioisha, kwamba anastahili mapumziko ya kutosha ili kuupa mwili wake nguvu.

“Kuna wachezaji ambao walicheza dakika nyingi, ili kuepusha miili yao isipate fatiki inawalazimu kuipumzisha miili yao, ili watakaporejea wawe na nguvu mpya, kuna kina Yao, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya,Dickson Job, Maxi Nzengeli na Djigui Diarra.

Aliongeza “Ukiachana hao, kuna wale ambao walipata na majeraha wakati Ligi Kuu inaisha hawakuwa na ufiti kama Khalid Aucho, Pacome Zouzou, hao nao programu yao ipo tofauti, wanakwenda kutafuta ufiti wa kujiweka sawa.

“Ukiacha hao wapo wale ambao walikuwa hawapati nafasi kubwa ya kucheza, nao watapaswa kupambana ili wakirejea wawe tayari kwa kutumika, maana utakuwa msimu wa kazi tu.”

Akizungumzia usajili unaoendelea amesema amekabidhi ripoti kwa viongozi wao ndio wanaofanyia kazi suala hilo la kusajili lakini anafuraha kuona wachezaji wake wote muhimu wameendelea kubaki ndani ya timu hiyo.

“Kazi yangu nimeikamilisha ni kuhakikisha nakabidhi ripoti haraka ili iweze kufanyiwa kazi hilo nimewaachia viongozi ambao tayari wamenihakikishia kubakiza mastaa wangu wote walionifanyia kazi nzuri msimu ulioisha,” alisema na kuongeza; “Endapo wataniongezea na wachezaji wa nafasi nilizopendekeza zifanyiwe kazi basi natarajia kuwa na msimu mwingine bora na naamini wachezaji hawataniangusha kuweza kufikia malengo,”alisema Gamondi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: