Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga haijakata tamaa ubingwa

7039e15bd4628d202061da82c0efdb4c Yanga haijakata tamaa ubingwa

Wed, 28 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UONGOZI wa Yanga umesema hawajakata tamaa ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwani bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michezo ijayo licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Jumapili iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Yanga ilifungwa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube dakika 85 na kuendelea kubaki katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 57 na Simba ikiwa kileleni kwa pointi 58 kabla ya mchezo wa jana.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Uhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz alisema ni matokeo mabaya waliyopata lakini benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mpya, Nasrideen Al Nabi limeanza kufanyia kazi makosa yaliyosababisha kichapo hicho.

Alisema kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC hakujawakatisha tama ya kuchukua ubingwa na kwamba ana amini wanachama na mashabiki wataendelea kuwa bega kwa bega na timu yao kama mwanzoni mwa msimu huu ambapo ilikuwa ikifanya vizuri.

“Hatujakata tamaa. Tuendelee kupambana kwenye kila mchezo kwa kila namna, ibakie kuwa ni matokeo ya mpira na bahati ya siku yenyewe.”

“Hapa lengo letu ni moja tu, kuendelea kupambana hadi pumzi yetu ya mwisho, na tunaamini tutapata tunachokikusudia, na hicho sio kingine zaidi ya ubingwa wa Tanzania Bara ambao tumeukosa kwa misimu mitatu mfululizo,” alisema Nugaz

Azam FC ina pointi 54 katika nafasi ya tatu na Yanga ikibaki na pointi 57 katika nafasi ya pili kwenye msimamo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz