Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga chupu chupu Nusu fainali Azam Sports Federation

Yanga Yatinga Nusu Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali kwa ushindi wa Penati 7-6

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo wa Soka nchini, Timu ya Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports mchezo uliopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa usiku huu.

Yanga wametinga hatua hiyo kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo.

Geita ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mtanange huo dakika ya 88 lililowekwa kimiani na Chikola baada ya kufanya Shambulizi la kustukiza kabla ya Djuma Shaban kuwasawazishia Yanga dakika za nyongeza na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Shujaa wa Yanga katika mchezo wa leo alikuwa ni golikipa Djugui Diarra aliefanikiwa kucheza mkwaju wa penati na kuwavusha Yanga kwa hatua ya Nusu Fainali.

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi alishuhudiwa akilimwa kadi nyekundu mara tu baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo.

Yanga wanasonga hatua ya nusu Fainali kwa ushindi wa Penati 7-6 na atamsubiri mshindi kati ya mechi ya Simba dhidi ya Pamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live