Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga chukueni hii, huu ndio mfumo wa Al Ahly ugenini

Al Ahly Medema Yanga chukueni hii, huu ndio mfumo wa Al Ahly ugenini

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mifumo mikubwa miwili ya Ahly wanayotumia ni 4-3-3 na ule ambao sawa na Yanga wanaoutumia wa 4-2-3-1 wakitegemea wanakutana na timu ipi.

Ilipokuja nchini mwezi uliopita kucheza dhidi ya Simba kwenye ufunguzi wa African Football League walitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao pia ulitumia na Wekundu hao wa Msimbazi tena kwenye mechi zote mbili, endapo Ahly akitumia mfumo huo kwa Yanga itakuwa ngumu kwao kushinda kutokana na wachezaji wengi wa Yanga kuwa na kasi zaidi wanapocheza kuliko Ahly.

Ahly wakiwa ugenini huwa hawatangulizi sana kushinda, hucheza kwa asilimia 60 pekee ikitegemea na ubora wa mpinzani huku wakitumia silaha la kujiangusha, kulalamika na kupoteza muda ili kupata sare jambo ambalo linaweza kuwasaidia Yanga ambao kwenye nafasi tatu ambazo wamekuwa wakipata mbili wamezitumia vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: